Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi wa mkoa wa Karbala wanaangalia namna ya kupanua mlango wa Bagdad

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar akiwa na mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswibu Jasim Khatwabi, wametembelea lango la Bagdad linalo elekea katika malalo mawili ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuangalia na kuweka mkakati wa upanuzi wake, ili kurahisisha matembezi ya mazuwaru hususan katika siku za ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Ziara hiyo imehusisha wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na wataalamu wake, pamoja na wawakilishi wa ofisi ya mkoa wa Karbala na ofisi ya wataalamu wa chuo kikuu cha Karbala.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ameongea kuhusu ziara hiyo, amesema kuwa: “Miongoni mwa majukumu ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni kurahisisha utembeaji wa misafara ya mazuwaru katika eneo la mlango wa Bagdad (Babu Bagdad) na maeneo ya jirani yake, leo tumetembelea sehemu hiyo tukiwa pamoja na mkuu wa mkoa na wadau wengine, kwa ajili ya kuweka mkakati wa kupanua barabara katika eneo hilo muhimu, ujenzi huo unatarajiwa kupunguza msongamano wa mazuwaru wanaokuja Karbala, tumekubaliana mambo kadhaa kuhusu ujenzi huo, kazi hii itaingizwa katika orodha ya kazi tulizo fanya kama vile ukarabati wa barabara ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na barabara zinazo elekea sehemu hiyo, kazi hiyo watapewa kamati ya wataalamu kutoka chuo kikuu cha Karbala, kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi kwa kuzingatia nafasi ya barabara hiyo”.

Mkuu wa ofisi ya Karbala Mhandisi Abiir Salim Naswiri amesema kuwa: “Tumefanya vikao vingi na Atabatu Huseiniyya na Abbasiyya tukufu pamoja na serikali ya mkoa, kujadili mkakati wa kuujenga mji huu na kuufanya uwe na muonekano mzuri, na barabara ni moja ya mambo ambayo hupendezesha mji, tutaanza kufanya upanuzi katika eneo la mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad), kwa sababu sehemu hiyo bado haijafanyiwa marekebisho tangu kuanguka kwa utawala uliopita, tutafanya kazi kwa timu pamoja na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kuwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na watumishi wa mkoa wa Karbala pamoja na wadau wengine katika mkoa wa Karbala, wanafanya kazi kwa pamoja muda mrefu katika miradi inayo lenga kuhudumia mazuwaru, walianza na mradi wa kukarabati barabara za mji mkongwe, kwa lengo la kupunguza msongamano wa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: