Kuanza kwa kazi ya kuandaa sakafu ya pambo la sega la Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuwekwa marumaru

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuanza kwa kazi ya awali katika kuweka marumaru kwenye sakafu tukufu ya pambo la sega ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi hiyo inafanywa sambamba na kuweka dhahabu kwenye kuta zinazo beba pambo hilo tukufu.

Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh rais wa kitengo tajwa ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi ya kuweka marumaru ni miongoni mwa kazi za mwisho katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi hiyo ilikamilika pamoja na kazi ya uwekaji wa dhahabu, halafu uwekaji wa marumaru ukaahirishwa hadi sasa, leo tumeanza kazi za awali kwa kutengeneza sehemu itakayo tiwa dhahabu ndani ya haram tukufu hadi sehemu inayo tenganisha baina yake na haram tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Kazi tutaigawa katika hatua tatu, tumeanza upande wa kulia wa pambo la dhahabu, itahusisha utowaji wa marumaru za zamani pamoja na vitu vingine vinavyo ambatana na marumaru, halafu tutaandaa ardhi kwa kuweka vitu maalum pamoja na nyaya za umeme na njia za mawasiliano, maji na mengineyo, kisha tutarudia kuweka marumaru sambamba na kuweka tabaka la chuma, na kuweka zege kwa kiwango kinacho endana na sakafu ya haram tukufu”.

Kumbuka kuwa kazi ya kuweka marumaru karika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ni miongoni mwa miradi inayo kamilisha miradi iliyo tangulia, unafanywa kutokana na kuharibika kwa marumaru za zamani, zilizo wekwa zaidi ya miaka (50) iliyo pita, jambo ambalo limepelekea kuharibika kutokana na umri wake, ndipo uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ukaamua kufanya mradi huu unao lenga kuongeza uzuri wa muonekano wa sehemu hii takatifu, kwa kiasi ambacho inatia furaha katika nafsi ya mtu anayekuja kufanya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: