Rais wa chuo cha Hamdaniyya amesema kuwa: Chuo kikuu cha Alkafeel ni uwanja mkubwa wa elimu ya sekula na kimesanifiwa kwa namna ambayo inaendana na historia ya mji wa Najafu Ashrafu

Maoni katika picha
Rais wa chuo kikuu cha Hamdaniyya katika mkoa wa Nainawa Dokta Aqiil Yahya Hashim Aáraji amesema kuwa Chuo kikuu cha Alkafeel ni uwanja mkubwa wa elimu unaofaa kujifaharishia, kimejengwa kwa namna ambayo kinaendana na turathi za mji wa Najafu.

Ameyasema hayo alipotembelea chuo kikuu cha Alkafeel kilicho chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kilichopo kwenye mkoa wa Najafu, alifuatana pia na rais wa chuo cha Kufa Dokta Yaasir Akiliy, wakapokelewa na rais wa chuo Dokta Nuuris Dahani na msaidizi wake wa elimu na wa utawala, pamoja na wakufunzi wa chuo.

Ugeni umetembelea korido za chuo na kumbi za madarasa pamoja na maabara, wakasikiliza maelezo kuhusu utaratibu wa masomo unaotumika.

Mwishoni mwa matembezi hayo wamekutana na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, wameonyesha furaha yao na kufungua milango ya ushirikiano kwa faida ya pande mbili na maslahi ya elimu hapa Iraq, wakaahidi kufanya ziara nyingine siku zijazo itakayo chochea ushirikiano kati ya vyuo vyetu.

Naye rais wa chuo cha Alkafeel Dokta Nuuris Dahani akasema: “Hakika milango ya chuo iko wazi kwa kila anayehitaji ushirikiano wa kielimu, ziara hii itaimarisha ushirikiano na chuo hiki pamoja na vyuo vingine hapa Iraq, vya serikali na binafsi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: