Chuo kikuu Alkafeel kimeratibu hafla ya wanawake ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) kwa mwaka wa tano

Maoni katika picha
Kwa mwaka wa tano mfululizo, chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla ya wanawake kusherehekea kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu na Mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w) kwa mwaka wa tano, ndani ya ukumbi wa Shekh Tusi na kuhudhuriwa na rais wa chuo hicho Dokta Nuuris Dahani na wasaidizi wake pamoja na wakufunzi, watumishi bila kusahau wanafunzi wa chuo hicho.

Mahafali imefunguliwa kwa Quráni tukufu na surat Faat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe wa Dokta Ali Shukriy, akasema: “Hakika mwanaadamu anamambo mawili makuu katika uhai wake, kuwa mwana Dini na kuwa na utukufu, na kuna jambo la tatu linakabiliana na hayo, nalo ni mataifa ya watu walio tangulia walikua wanatukuza wanachuoni wao, na sisi tunamtukuza na kuadhimisha kutokana na misingi bora ya ubinadamu aliyo fundisha, hakika Mtume Muhammad (s.a.w.w) amefundisha Dini inayo heshimu ubinaadamu wa kila mtu, Dini yenye sheria na hukumu za uadilifu”.

Yakafuata mashairi kuhusu kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) aliye kuja kuwatoa binaadamu wote kwenye giza na kuwatia katika nuru.

Shekh Husam Abedi rais wa kitengo cha kuongoza nafsi na muongozo wa malezi katika chuo kikuu hicho amesema kuwa: “Kufanya hafla hii ni sehemu ya vipaombele vya chuo katika kuhuisha matukio ya Dini kwa ajili ya kuelekeza familia kwenye njia ya haki na mwenendo wa Ahlulbait (a.s), hususan wakati huu ambao dunia inamkosea heshima Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: