Chuo kikuu cha Al-Ameed kimetangaza kanuni za kukubaliwa kujiunga na masomo katika chuo chake kwa mwaka wa masomo (2020 /2021m)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza masharti ya kukubaliwa katika vitivo vyake, (Udaktari – udaktari wa meno – famasia na uuguzi) kwa mwaka wa masomo (2020 / 2021m).

Maombi yatumwe kwa njia ya mtandao maalum uliotangazwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, ambao unaorodha ya vyuo vikuu pamoja na garama zake kwa kila kitivo, kama ifuatavyo:

  1. Kitivo cha udaktari kiwango cha chini %92.
  2. Kitivo cha udaktari wa meno kiwango cha chini%83.
  3. Kitivo cha famasia kiwango cha chini %83.
  4. Kitivo cha uuguzi kiwango cha chini %60.

Kwa maelezo zaidi piga namba za simu zifuatazo:

(07733078000) (07817448000) (076‪024‪180‪00) au tembelea toghuti hii https://alameed.edu.iq/

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed ni taasisi ya elimu iliyo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesajiliwa na wizara ya elimu na utafiti wa kielimu hapa Iraq, inavitivo vifuatavyo (kitivo cha udaktari – kitivo cha uuguzi na kitivo cha meno), kilifunguliwa kitivo cha kwanza cha udaktari kwa kufuata kiwango cha vituo binafsi vya Iraq, kikaboreshwa kuhakikisha kinakua kimbilio la kielimu ukilinganisha na vyuo vikuu vingine, kinatumia mifumo ya kimataifa inayo kiwezesha kuingia katika ubora unaokubalika, chuo kipo katika mkoa wa Karbala – mwanzo wa barabara ya –Karbala – Najafu- karibu na nguzo namba (1238).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: