App ya Haqiibatu Mu-uminu inawatumiaji zaidi ya milioni (12) na inafanya vizuri

Maoni katika picha
App ya Haqiibatu Mu-uminu iliyo tengenezwa na idara ya teknolojia na taaluma ya mitandao katika kitengo cha habari ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inawatumiaji milioni (12) kutoka nchi tofauti duniani, kutokana na vitu ilivyo navyo imekua App maarufu ya kiislamu duniani.

Msimamizi wa App hiyo amesema kuwa: “App ya Haqiibatu Mu-uminu ambayo ni miongoni mwa App za kiislamu imefanikiwa kushinda App nyingi za mfano wake, hii inatokana na mbinu madhubuti zinazo tumika katika kupanga maudhui zinazo jibu matatizo mengi ya waislamu kote duniani”.

Akaongeza kuwa: “Wazo la kuanzishwa kwa App ya (Haqiiibatu Mu-uminu) ambayo ndio App maalum ya kwanza kuanzishwa kwenye simu za kisasa (smatphone), iliwekwa kila kitu anacho hitaji Muumini katika mambo ya ibada, kama vile swala, kusoma Quráni, kusoma dua, alam za nyakati za adhana na mengineyo, ilitengenezwa na kupangiliwa kwa ujuzi mkubwa, ilianza mwaka (2014), wataalam wanao simamia App hiyo wamekua wakiiboresha kila wakati, sambamba na kuifanya iendane na maendelea yanayo patikana katika sekta hiyo, aidha maoni ya watumiaji yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuiboresha App hiyo”.

Akafafanua kua: “App hiyo imekubalika kwa kiasi kikubwa sana katika App za kiislamu duniani, imepata kiasi cha (4.8) kwa kuwa na wafuatiliaji zaidi ya (325,000) huku watumiaji wakiwa zaidi ya milioni kumi, hakuna App yeyote hapa Iraq iliyokuwa na idadi kubwa sawa na hiyo ya watumiaji hapa Iraq”.

Akaashiria kuwa: “Takwimu za watu wanao pakua App hiyo zinaendelea kupanda kila siku, kama ifuatavyo:

Google play 10,223,409.

Haway stor 178000.

Apol stor (I phone) 1,424,131.

Ili kupakua App hiyi ingia hapa http://bit.ly/2tzCvDD
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: