Kitivo cha famasia katika chuo kikuu cha Al-Ameed kimewasha mshumaa wa kwanza na kuwazawadia wanafunzi wake waliopata nafasi za kwanza

Maoni katika picha
Viongozi wa kitivo cha famasia katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, asubuhi ya Jumamosi (27 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na (14 Novemba 2020m) wamefanya hafla ya kumaliza mwaka tangu kuanzishwa kwake katika chuo hicho.

Hafla hiyo imefanywa katika bustani ya chuo na kuhudhuriwa na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na wasaidizi wake, bila kusahau walimu na wanafunzi wa kitivo hicho pamoja na vitivo vingine, na ugeni uliowakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kurehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa). Baada ya hapo ukawashwa mshumaa mmoja ukimaanisha ndio umri wa kitivo hicho kinacho toa elimu na kutarajiwa kuongeza wasomi wenye viwango bora kabisa hapa nchini.

Hafla hiyo pia imeshuhudia kupewa zawadi kwa wanafunzi watatu walioshika nafasi za kwanza katika mitihani ya mwaka jana, zawadi hizo zimekabidhiwa na rais wa chuo na msaidizi wake, baada ya hapo wahudhuriaji wakaenda kwenye ufunguzi wa maonyesho yaliyo andaliwa na wanafunzi wa chuo, yaliyo kuwa na mabango ya kuchorya kwa mikono kama sehemu ya kuonyesha vipaji vyao katika fani hiyo.

Mwisho akapewa zawadi mkuu wa kitivo cha famasia Dokta Ahmadi Hashim Rifaai, kama sehemu ya kuonyesha kuthamini kazi kubwa anayo fanya katika mazingira magumu kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: