Katika mradi wa Arshu-Tilawa: Aya na usomaji wa Quráni unaendelea ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya vikao vya usomaji wa Quráni ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa jina la (Arshu-Tilawa) na kusimamiwa na kituo cha miradi ya Quráni katika Maahadi hiyo.

Wameanza kwa Quráni tukufu iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Haani Mussawi.

Akafuatia Haafidh Mahadi Ridhwa Salam mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Quráni unao simamiwa na Maahadi, wakati wa usomaji wake ameonyesha kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu, kwa kutaja namba za kurasa, aya, zujuu na majina ya sura, sambamba na kusoma aya kwa kuanzia nyuma (kurudi nyuma).

Baada yake akafuatia msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu Liith Ubaidi na mwisho akazungumza Dokta Munjid Kaabi, kupitia utaratibu wa usomaji wa Quráni na maarifa yanayo patikana katika aya za Quráni na hadithi za Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), huzungumzwa mada tofauti kila wiki, mada iliyo tolewa na Shekh Kaabi inahusu kufanya biashara na Mwenyezi Mungu na sifa za waumini katika Quráni, huku Abulfadhil Abbasi (a.s) akiangaliwa kama mfano na msingi wa mada yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: