Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekungu imesema kuwa: Usia wa Marjaa Dini mkuu ni kielelezo cha amani kwa watu wa tabaka zote katika jamii

Maoni katika picha
Rais wa tawi la msalaba mwekundu katika mkoa wa Najafu bibi Maryam Laya Milra amesema kuwa usia uliotolewa na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani wakati wa vita ya Iraq ulifanikiwa kurudisha ardhi yao iliyokua imetekwa na magaidi wa Daesh, unazingatiwa kuwa kielelezo cha amani kwa raia wote wa Iraq.

Hayo yamesemwa katika ziara iliyofanywa na Milra pamoja na ujumbe wake katika ofisi ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Liwaau/26 Hashdu-Shaábi, na kupokelewa na kiongozi mkuu wa kikosi hicho Maitham Zaidi, wakazungumza mambo mbalimbali kuhusu kazi zinazo fanya na kamati hiyo, Zaidi akazungumza mambo muhimu yaliyofanywa na kikosi pamoja na mchango wao katika kulinda amani ya taifa, akasisitiza kuwa: “Kikosi kinafanya kazi za aina mbili, kina sekta ya misaada ya kibinaadamu, kama vile kusaidia familia za wakimbizi na mafakiri sambamba na kusaidia taasisi za serikali zinazo toa huduma za kijamii, na sekta ya pili ni kulinda amani, sekta hiyo imeweka askari kila sehemu kwa ajili ya kupambana na magenge ya kigaidi na kihalifu hapa nchini”.

Akabainisha kuwa kikosi kipo tayali kushirikiana na chama cha msalaba mwekundu katika maeneo yote kinayo fanya kazi.

Mwishoni mwa kikao hicho wageni wamekishukuru kikosi cha Abbasi kutokana na kazi kubwa kinazo fanya na wakaahidi kutoa ushirikiano katika vituo vya kikosi, sambamba na kushukuru ushirikiano uliotolewa na kikosi hicho siku za nyuma, kupitia makongamano mbalimbali ya kujadili misaada ya kibinaadamu, hali kadhalika kutakuwa na kongamano lingine hivi karibuni la kujadili kazi zinazo fanywa na kikosi na umuhimu wa amani na kujiepusha na vita na vurugu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: