Haya yamebainishwa na mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim, akasema kuwa: “Kutokana na riwaya ya kwanza inayo taja kifo cha bibi Zaharaa (a.s), semina hii itachukua siku tatu kupitia jukwaa la mtandao wa telegram kwa link ifuatayo: https://t.me/Alzahraaealahaalsalam
Kuanzia mwezi (7 Rabiul-Aakhar) hadi mwezi tisa, wahadhiri wabobezi watafundisha kwenye semina hiyo, aidha kutakuwa na nafasi ya maswali na majibu”.
Akabainisha kuwa: “Mada za semina zitakua kama zifuatavyo:
- - Nguvu ya mtu binasfi ni siraha kubwa, ni ipi misingi ya nguvu binafsi? Bibi Zahara kama mfano.
- - Katika kuangazia historia ya Zaharaa (a.s), kuhusu utatuaji wa matatizo ya familia.
- - Umama ni moja ya jambo muhimu katika maisha ya mwanamke, jambo hilo huimarishwa kwa kuwa na upendo na upole, tunayaona hayo kwa bibi Zaharaa (a.s), namna gani tutajaza mapenzi kwa watoto wetu kwa kufuata mwenendo wa bibi Fatuma?
- - Wanandoa watukufu Ali na Fatuma (a.s) Mwenyezi Mungu amewafanya kuwa kiigizo chema kwa watu wote, namna gani tunaweza kunufaika nao katika kutatua matatizo ya ndoa zetu?”.