Nadwa katika kumbukumbu ya kifo cha Swidiqah Fatuma Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Katika kukumbuka fadhila za Ahlulbait (a.s), Maahadi ya Quráni tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya nadwa ya kukumbuka kifo cha Swidiqah Fatuma Zaharaa (a.s), yenye anuani isemayo (Swalawatu Muhammadiyyah wal-maqamaatu Fatwimiyyah), mtoa mada wa nadwa hiyo ni mwalimu wa hauza bi Ruqayyah Muhammad Ridhwa Sharifu, itafanywa kwa njia ya mtandao kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, siku ya Jumanne tarehe (24 Novemba 2020m) saa tatu jioni kupitia program ya (meet) kwa link ifuatayo: (https://meet.googel.com/jep-zzcj-cvo).

Ustadhat Mannaar Jaburi kiongozi wa Maahadi amesema kuwa: “Hakika kufanya matukio maalum ya kuwakumbuka Ahlulbait (a.s) ni sehemu ya majukumu ya Maahadi ya Quráni, kwa sababu Ahlulbait (a.s) ni sawa na Quráni, wao na kitabu cha Mwenyezi Mungu ndio vizito viwili alivyo usia Mtume (s.a.w.w) kushikamana navyo, hivyo Maahadi inatilia umuhimu mkubwa kuadhimisha matukio yanayo husu Ahlulbait (a.s) kwa ajili ya kupata mafunzo na mazingatio kutoka katika historia ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) na maneno yao matukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: