Semina ya (kuboresha ofisi) katika Atabatu Abbasiyya yaingia siku ya tano

Maoni katika picha
Semina ya (kuboresha ofisi) imeingia siku ya tano, zinafundishwa njia za kisasa za uongozi kwa marais wa vitengo na wakuu wa mashirika yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kuongeza uwezo wa kuongoza ofisi na kutumia mbinu za kisasa zinazo tumiwa na taasisi za kimataifa.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Maitham Zaidi amesema kuwa: “Hakika mafunzo haya ni muhimu sana kwa viongozi na yanaendana na wajimu wa Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Kuna haja ya kuendelea kupata mafunzo haya, kwa sababu ofisi ya mtu vyovyote itakavyo kuwa na mafanikio bado itahitaji kuboreshwa zaidi, ili kuifanya iendane na maendelea yaliyopo katika uwanja wa kazi, ukizingatia kuwa idadi ya mazuwaru inaongezeka kila mwaka sambamba na utoaji wa huduma”.

Naye rais wa kitengo cha habari na utamaduni dokta Sarhani Jafati Salmani amesema kuwa: “Hakika mwanaadamu katika kila sekta ya maisha yake anahitaji kuongeza uwezo na kuboresha elimu, bila shaka kila semina inayolenga kuongeza uwezo ni muhimu, semina hii ya kujenga uwezo na kuongeza maarifa ni muhimu sana, kwani inawafanya watumishi kutambua mbinu mpya”.

Akafafanua kuwa: “Hakika semina hii inamuwezesha mshiriki kupata elimu nyingi za nadhariya, anayo nufaika nayo katika kuamiliana na watumishi kwa mbinu mpya za kiidara, pamoja na mambo ambayo hayakuwepo zamani, ikiwa ni pamoja na kuboresha ofisi na kuwa na utendaji wa kisasa unao endana na zama hizi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: