Mafundi wa kitengo cha majengo ya kihandisi wanamalizia kujenga sakafu ya hospitali ya Hindiyya

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wanamalizia kujenga sakafu ya hospitali ya Hindiyya katika mkoa wa Karbala, kazi hii ni sehemu ya miradi ya kibinaadamu inayo fanywa na Ataba tukufu, katika kusaidia sekta ya afya na majengo yake.

Kiongozi wa idara ya ujenzi inayo simamia ujenzi huo Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawiil amesema kuwa: “Kazi za kitengo chetu haziishii katika Atabatu Abbasiyya peke yake, japokuwa hilo ndio jukumu kuu, kuna kazi zingine huwa tunapangiwa na uongozi mkuu wa Ataba tukufu, kutokana na maombi ambayo hupokea, hususan yanapokuwa yanauhusiano wa moja kwa moja na huduma kwa wananchi ikiwemo sekta ya afya”.

Akaongeza kuwa: “Eneo la sakafu ya uwanja wa hospitali lililo jengwa kwa ajili ya kuzuwia maji ya mvua yasiingie katika hospitali linaukubwa wa (mt 1750), tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kazi imekamilika ndani ya muda mfupi”.

Kumbuka kuwa kazi ya kujenga sakafu ni sehemu ya miradi ya kibinaadam inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kujenga na kukarabati baadhi ya majengo ya serikali yaliyo haribika, tayali tumesha fanya ukarabati katika shule nyingi, taasisi za kibinaadamu, hospitali na sehemu zingine zinazo toa huduma kwa wananchi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: