Rais kutoka chuo kikuu cha Basra amesema kuwa: Tunatarajia kufanya makubaliano na chuo kikuu cha Alkafeel katika sekta ya elimu na teknolojia

Maoni katika picha
Mgeni kutoka chuo kikuu cha Basra Dokta Kiyani Sabahi makamo wa mkuu wa kompyta katika chuo kikuu hicho, ameonyesha nia ya kufanya makubaliano na chuo kikuu cha Alkafeel katika sekta ya elimu na teknolojia.

Dokta Kiyani ametembelea chuo kikuu cha Alkafeel akiwa pamoja na rais wa chuo kikuu cha Basra Dokta Saádi Shahin Hamadi, wametembelea sehemu mbalimbali za chuo, wamepokelewa na rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuuris Muhammad Shahidi na baadhi ya wakuu wa vitengo vya chuo na wakufunzi.

Dokta Kiyani amefurahishwa na majengo ya chuo pamoja na kumbi za madarasa na maabara zake, ikiwa ni pamoja na utaratibu wa ukaaji wa wanafunzi kwa umbali unaotakiwa na idara za afya kati ya mtu na mtu pamoja na kuzingatia masharti yote ya kujikinga na virusi vya Korona vinavyo sumbua dunia kwa sasa, sambamba na kukidhi vigezo vya kitaifa.

Dokta Kiyani Sabahi amepongeza utaratibu na teknolojia inayo tumiwa na chuo katika utoaji wa elimu, amesema kuwa ni utaratibu bora kabisa katika vyuo vikuu vya Iraq, unakidhi kila anacho hitaji mwanafunzi na mwalimu katika kusoma na kusomesha.

Baada ya ziara yao akasema kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kinauzowefu mkubwa na mbinu nzuri zinazo faa kuigwa na vyuo vikuu vyote vya Iraq, sawa viwe vya serikali au binafsi, kutokana na maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na teknolojia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: