Mawakibu za kutoa misaada zimefanya kongamano la kwanza

Maoni katika picha
Mawakibu za kutoa misaada katika mkoa wa Diyala chini ya kitengo cha ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu zimefanya kongamano la kwanza lenye kauli mbiu isemayo: (Mawakibu Husseiniyya ni ukarimu usioisha upya wake), na kuhudhuriwa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Ustadh Maitham Zaidi, na wawakilishi wa mawakibu na viongozi wa kidini, kijamii na kikabila pamoja na viongozi wa ofisi za ustawi wa jamii kutoka mikoa tofauti.

Kongamano limefanyiwa ndani ya ukumbi wa mgahawa (mudhifu) wa Imamu Hussein (a.s) na kufunguliwa kwa Quráni tukufu pamoja na kisomo cha surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ukafuata ujumbe wa Ustadh Zaidi ambae amepongeza kazi nzuri inayofanywa na mawakibu hizo, zikiwemo mawakibu za mkoa wa Diyala, sawa iwe katika kusaidia askari wa serikali au Hashdu-Shaábi au misaada ya kibinaadamu ambayo hutolewa kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, ulimi hauwezi kuongea yote na maneno hayatoshi kutoa pongezi kwa mawakibu hizi kutokana na ukarimu wao, akaomba waendelee na moyo huohuo.

Baada ya hapo ikaonyeshwa filamu yenye matukio ya misaada iliyotolewa na mawakibu hizo hapa mkoani, na mwisho wa kongamano wawakilishi wa mawakibu wakapewa zawadi kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kama sehemu ya kuonyesha thamani ya kazi zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: