Chuo kikuu cha Al-Ameed kimetoa muongozo wa ubora na kimesisitiza kuwa kitasimamia ubora katika taasisi za elimu

Maoni katika picha
Hivi karibuni kitengo cha kudhibiti ubora katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa kitabu cha (muongozo wa ubora katika chuo kikuu cha Al-Ameed), nacho ni toleo la kwanza katika matoleo ya (vitabu vya ubora), hii inatokana na chuo kufuatilia maendeleo yanayo patikana kwenye taasisi za elimu, na kulinda maendeleo yanayo patikana ndani na nje ya chuo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Muhammad Swalaal Khazrajiy rais wa kitengo cha kudhibiti ubora wa chuo, amesema: “Muongozo huo unatokana na ukubwa wa sekta ya elimu ya sekula, chini ya msaada wa rais wa chuo, kwani analipa umuhimu mkubwa swala hili, kitabu hicho cha muongozo kina sehemu tano kama ifuatavyo:

Sehemu ya kwanza: Dira ya chuo na malengo yake.

Sehemu ya pili: Kubainisha ubora katika chuo kikuu cha Al-Ameed na muundo wake.

Sehemu ya tatu: Kuangalia maana ya ubora na uelewa wake.

Sehemu ya nne: Kujadili mafuhumu ya ubora na kutambua nani anayewajibika na ubora katika chuo, na misingi ya ubora katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Sehemu ya tano: Kufanyia uhakiki wa (Mafuhumu ya misingi ya ubora na mikakati ya utekelezaji).

Akamaliza kwa kusema: “Hakika kitabu hiki kinaweza kutumiwa na vitivo vya chuo pamoja na vitengo vyake, kutokana na umuhimu wa kueneza ubora kwenye taasisi zote za ubora hapa nchini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: