Kufunga screen kubwa ya pande mbili katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Idara ya mawasiliano na teknolojia chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kumaliza uwekaji wa Screen kubwa la kisasa yenye uwezo mkubwa na inapande mbili, kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu upande wa mlango wa Imamu Hassan (a.s), na kuchukua nafasi ya Screen iliyokuwepo zamani, limeondolewa bango la zamani kwa sababu lilikuwa na teknolojia ya zaidi ya miaka 10 iliyopota.

Kiongozi wa idara ya uhandisi bwana Farasi Hamza ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Miongoni mwa mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuingiza teknolojia mpya, na kuzitumia chini ya misingi ya kiislamu kwa ajili ya mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuchangia kufikisha fikra kwa kila mdau na zaairu wa eneo hili takatifu, tumefanya kazi ya kuweka Screen mpya kutokana na faida tulizo ziona katika Screen ya zamani”.

Akaongeza kuwa: “Hakika Screen inaubora mkubwa, ni miongoni mwa Screen chache zilizopo Iraq, inamambo yafatayo:

  • - Ni kubwa kushinda Screen ya zamani, inaurefu wa (mt 3.84) na upana wa (mt 6.4), jumla ukubwa wake unakadiriwa kuwa (mt 25).
  • - Linatumia teknolojia ya (DIP 3 in 1) ambayo ni teknolojia ya kisasa zaidi duniani.
  • - Linapande mbili na zote zinaonyesha picha zenye ubora mkubwa.
  • - Kioo chake kina uwezo wa (8000) wa mwanga, nao ni uwezo mkubwa ukilinganisha na Screen za aina hiyo, picha zake zinaonekana vizuri hata mchana.
  • - Inapokea taarifa za kielektronik kupitia kebo ya mwanga iliyo unganishwa na kituoa cha ukaguzi katika idara ya mawasiliano.
  • - Inapozwa kwa kutumia hewa peke yake wala haihitaji kiyoyozi kwa ajili ya kuipoza hivyo inatumia umeme mdogo.
  • - Inapo washwa hutumia umeme kidogo sana tofauti na Screen iliyokuwepo zamani.
  • - Inauwezo mkubwa wa kuvumilia mazingira yote ya hewa hadi nyuzi tote 75”.

Akaendelea kusema: “Screen imefungwa juu ya nguzo zilizo simikwa ardhini kwa uhodari mkubwa, na imefungamana na Screen zingine zilizopo ndani ya haram tukufu, kwa ajili ya uhakiki wa maudhui na taarifa zinazo onyeshwa kwenye Screen hiyo”.

Kumbuka kuwa Screen ni moja ya nyenzo za kisasa zinazo tumika kuonyesha aya za Quráni tukufu na hadithi za Mtume pamoja na usia wa maimamu wa Ahlulbait (a.s) sambamba na mafundisho mbalimbali ya kiislamu yenye manufaa kwa mazuwaru, ili kuwafanya waweze watekeleze ibada ya ziara kwa ukamilifu na baadhi ya wakati hutumika kutoa maelekezo maalum ya afya hasa kuhusu janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: