Kuanza kilimo cha ngano zenye ubora mkubwa katika mradi wa Saaqi wenye ukubwa wa dunam (1000)

Maoni katika picha
Watumishi wa mradi wa Saaqi (kilimo) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza kulima ngano zenye ubora wa hali ya juu katika shamba lenye ukubwa wa dunam (1000), baada ya kumaliza maandalizi ya lazima kwenye eneo la shamba hilo, tena kwa kutumia njia za kisasa.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maandalizi ya msimu wa kilimo cha masika yamesha anza, tumesafisha shamba na kuondoa mabaki ya mwaka jana, pamoja na kufanya matengenezo makubwa kwenye mashine zote za umwagiliaji zipatayo (11), mashine (8) katika hizo zinauwezo wa kumwagilia dunam (80) kila moja, na mashine (3) kila moja inaweza kumwagilia dunam (120), kilimo kimefanywa kwa kutumia mitambo ya kisasa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tunatarajia kilimo hiki kuwa na mafanikio makumbwa kama kilimo kilicho tangulia”.

Mkuu wa mradi huu Ustadh Zaki Swahibu amesema kuwa: “Shamba tunalo lima linaukubwa wa dunam (1000) tunalima ngano zenye ubora mkubwa wa kiwango cha (Ibaa 99), na kutumia njia ya umwagiliaji kwenye kila dunam, na kuweka mbolea ya samadi tani (6 – 7) kwenye kila dunam moja, jumla ya mashine (5) za umwagiliaji zimetumika kila moja katika eneo lake maalum, limeboreshwa sana eneo la shamba mwaka huu na kuongezwa mashine mbili za umwagiliaji, ni sehemu ya mkakati wa kuongeza eneo zaidi la shamba, na kulitumia kwa kilimo cha ngano ambacho kipo ndani ya mkakati wa Ataba tukufu”.

Kumbuka kuwa mradi wa Saaqi ni moja ya miradi ya kimkakati, inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kutumia jangwa la mkoa wa Karbala, na kupanda mazao ya kimkakati likiwemo zao la ngano, kwa lengo la kujenga kujitegemea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: