Kitengo cha Dini kimetoa mhadhara wa kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeratibu mhadhara wa kuomboleza kifo cha pande la damu ya Mtume bibi Zaharaa (a.s), kwa mujibu wa riwaya ya kwanza ya kifo chake ambayo siku ya kifo chake inasadifu siku ya leo mwezi nane Rabiul-Aakhar.

Mhadhara umetolewa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na idadi maalum ya mazuwaru, waliokaa kwa umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu, mzungumzaji alikua ni Shekh Muhsin Asadi na ameeleza mambo mengi, amesimulia historia ya Swidiiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s) na msimamo wake wa kishujaa katika kupinga dhulma na kutetea haki, akasisitiza ulazima wa kufuata mwenendo wake na kupambika kwa tabia zake (a.s), akakumbusha uhusiano mkubwa uliopo kati ya Ahlulbait (a.s) na Quráni tukufu, na umuhimu wa kujitahidi kufahamu mafundisho ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, akataja dhulma kubwa aliyofanyiwa bibi Zaharaa (a.s) na jinsi alivyo jitolea katika kutetea ujumbe wa Mwenyezi Mungu, kabainisha mchango wake katika kujenga misingi ya Dini ya kiislamu, akahitimisha kwa kusoma tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni kufuatia kifo hicho na yaliyo tokea baada ya kifo chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: