Masayyid wanaomboleza kifo cha bibi yao Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameomboleza kifo cha bibi yao Fatuma Zaharaa (a.s) (kwa mujibu wa riwaya ya kwanza), wanafanya majlisi za kuomboleza ndani ya siku tatu, chini ya uhadhiri wa Shekh Ali Mujaan kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amemzungumzia bibi huyo mtakatifu na athari zake pamoja na mambo aliyo ufanyia uislamu, na heshima kubwa aliyo kuwa nayo kwa baba yake (s.a.w.w).

Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Hashim Shami kiongozi wa masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya amesema kuwa: “Yanafanywa katika ukumbi wa Aljuud (uwanja uliopo mkabala na mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi a.s), saa kumi jioni ndani ya siku tatu mfululizo, na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona ikiwa ni pamoja na kuzingatia ukaaji wa umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu, majlisi hizo zinahudhuriwa na mazuwaru pamoja na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akasema: “Hakika majlisi hii inafanywa kwa mwaka wa kumi na tatu, nayo ni sehemu ya harakati za kitengo hiki ya kuhuisha matukio ya kidini, katika kuadhimisha matukio ya kusikitisha kwa Ahlulbait (a.s), likiwemo tukio hili la kifo cha bibi Zaharaa (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: