Mihara ya kidini na kufanya majlisi za kuomboleza ni sehemu ya utaratibu wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika siku za Fatwimiyya

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa utaratibu wake ni kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza, imefanywa majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram tukufu siku ya Jumanne jioni mwezi (8 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (24 Novemba 2020m).

Majlisi ilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyosomwa na msomaji wa Ataba mbili Sayyid Hasanaini Halo, baada yake Shekh Abdullahi Dujaili akapanda kwenye mimbari na kutoa mhadhara kuhusu historia ya bibi Zaharaa (a.s) na nafasi yake katika uislamu pamoja na heshima kubwa aliyonayo kwa baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kueleza dhulma aliyo fanyiwa (a.s).

Halafu muimbaji mashuhuri bwana Baasim Karbalai akapanda kwenye mimbari na kuimba tenzi zilizo onyesha ukubwa wa msiba huu na huzuni waliyonayo waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: