Maktaba ya wanawake imeratibu warsha ya kitamaduni kuhusu utatuzi wa matatizo na kuchukua hatua

Maoni katika picha
Maktaba ya wanawake chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa warsha kwa watumishi wake chini ya anuani isemayo: (kubaini matatizo na kuchukua hatua), warsha hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa Iárah na mtoa mada alikuwa ni Ustadhat Suzan Mikdadi kutoka Lebanon, ili kuwajengea uwezo watumishi na maarifa zaidi, hiyo ndio kawaida ya maktaba, imeshafanya warsha na semina za aina mbalimbali kwa watumishi wake.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa maktaba ya wanawake bibi Asmaa Raádu, akaongeza kuwa: “Warsha imejikita katika mambo muhimu yanayo endana na anuani ya warsha hii, ikiwa ni pamoja na namna ya kubaini tatizo na njia za kutumia, imepata muitikio mkubwa na imekubalika sana kwa washiriki”.

Bibi Hauraa Hassan Hashimi muandisi wa jarida la Riyadhu-Zaharaa (a.s) na mmoja wa washiriki wa warsha hiyo, amesema kuwa: “Warsha imejikita katika mambo muhimu ukizingatia kuwa inahusiana na mkakati wa kutatua changamoto, jambo ambalo huwa halitokea kwa urahisi, linategemea mbinu utakazo tumia, na kuhakikisha tatizo halisambai sehemu zingine, tumepata faida kubwa katika warsha hii”.

Tambua kuwa Ustadhat Suzan Mikdadi ametembelea maktaba na kuangalia huduma zinazo tolewa kwa njia ya mtandao na kwa wageni wanaoingia maktaba, amesifu utendaji wa watumishi wake na kusema kuwa wanafanya kazi kwa ushirikiano mzuri kama nyuki.

Kumbuka kuwa idara ya maktaba ya wanawake ipo tayali kunufaika na kila mtu katika kuboresha utendaji wake, imepiga hatua kubwa katika sekta hiyo, na imeonyesha matunda katika utendaji na kuifanya kuwa maktaba yenye maendeleo makubwa miongoni mwa maktaba za wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: