(Mtume Muhammad -s.a.w.w- na Mayahudi wa Madina.. mazingira ya uhusiano na maendeleo yake kwa mujibu wa Quráni) anuani ya nadwa ya Multaqa Siraratu-Nabawiyyah

Maoni katika picha
Daru Rasulul-A’dham (s.a.w.w) chini ya kituo cha Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat/ kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya nadwa kuhusu historia ya Mtume mtukufu, iliyopewa anuani ya (Mtume Muhammad –s.a.w.w- na Mayahudi wa Madina.. mazingira ya uhusiano na maendeleo yake kwa mujibu wa Qurni) jioni ya Ijumaa mwezi (11 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na (27 Novemba 2020m) kupitia jukwaa la (ZOOM), mhadhiri wa nadwa hiyo alikuwa ni Dokta Mushtaqu Bashiri Ghazali na washiriki wengi walikuwa ni wasomi wa sekula na watafiti wa mambo ya historia.

Katika nadwa hiyo yamejadiliwa mambo mengi muhimu kuhusu historia ya Mtume mtukufu (s.a.w.w) na kuyalinganisha na Quráni tukufu, mhadhiri ameangazia sehemu muhimu katika historia ya Mtume, sehemu yenye utata mwingi hususan katika mapokezi ya kiislamu yanayo tumiwa na Mustashriqina, walio andika kwenye vitabu vyao makosa na mambo yasiyofaa katika historia ya Mtume hasa kuhusiana na jinsi alivyo ishi na mayahudi wa Madina, na kwa namna yapekee jinsi alivyo wachukulia Bini Quraidhwa, kwenye vitabu vya Mustashriqina utakuta makosa na mambo yasiyofaa kwa Mtume (s.a.w.w) yako wazi wazi.

Mhadhiri akaonyesha hali halisi ya Mustashriqi kuwa misingi ya mapokezi yao haina uhalisia, wanategemea mapungufu yaliyopo katika baadhi ya mapokezi ya kiislamu, kwani baadhi za riwaya zinamapungufu ya wazi, hivyo wameshikilia riwaya hizo na kunufaika nazo kwa kutoa pisha potofu na isio hahihi.

Akasisitiza kuwa ni wajibu wetu kuangalia swala hili na kubaini mapungufu yaliyopo katika riwaya za kiislamu, ili tuweze kuonyesha uhalisia wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Mwisho wa nadwa hiyo ukafunguliwa mlango wa majadiliano na maswali, Uatadh Gazali akajibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale alipo hitajika kufanya hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: