Bidhaa za Alkafeel zimepata nafasi ya mashirika makubwa katika tamasha la biashara la kimataifa mjini Basra

Maoni katika picha
Shirika la Nurul-Kafeel linalotengeneza bidhaa za chakula, limeshiriki kwenye tamasha la sita la kibiashara na kimataifa mjini Basra, ambalo limeanza katikati ya wiki hii chini ya usimamizi wa shirika kuu la maonyesho na huduma za kibiashara Iraq, katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa mkoani Basra na kushiriki mashirika (100) ya kitaifa na kimataifa, kutoka Misri, India, Tajikistan, Moroko, Jodan na Iran.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa shirika hilo Ustadh Bahaau Hamidi Saudi, amesema: “Ni moja ya tamasha nyingi tulizo hudhuria na kupata mwitikio mkubwa, matawi ya shirika yanabidhaa mbalimbali kama vile nyama, nyekundu na nyeupe, mafuta, mchele, tomate za kopo na viungo vingine vya kusindikwa kwenye makopo, vinaubora unaokidhi vigezo vya kimataifa, sambamba na kutimiza masharti yote ya taasisi ya vipimo na ubora ya Iraq, tawi letu limevutia sana watu wanaokuja kutembelea tamasha hili miongoni mwa familia za raia wa Iraq pamoja na washiriki wa tamasha”.

Akaongeza kuwa: “Tawi la bidhaa za Alkafeel ni sawa na kiunganishi kati ya wateja na shughuli zinazo fanywa na shirika ikiwemo bidhaa wanazo tengeneza ambazo ni kimbilio la familia nyingi za wairaq, watu waliotembelea tawi letu wamepongeza na kusifu bidhaa tunazo tengeneza na kusema kuwa zinakidhi haja ya wananchi”.

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye tamasha hili ni sehemu ya utaratibu wa kushiriki kwenye matamasha ya kitaifa na kimataifa ambayo ni sehemu muhimu ya kukutana na walaji (wateja) wa bidhaa zetu moja kwa moja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: