Madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kuondoa uvimbe kwenye goti la mgonjwa mwenye umri wa miaka thelathini

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kuondoa uvimbe kwenye goti la mgonjwa mwenye umri wa miaka thelathini, upasuaji umefanywa kwa kutumia teknolojia ya (Nadhuur).

Daktari bingwa wa kuunganisha sehemu zilizo vunjika na viungo vya mwanaadamu katika hospitali ya rufaa Alkafeel Dokta Ahmadi Ni’mah, amesema kuwa: “Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kuondoa uvimbe kwa kutumia teknolojia ya (Nadhuur) kwenye koti la mgonjwa mwenye umri wa miaka (30)”.

Akaongeza kuwa: “Tumefanikiwa kuondoa uvimbe wote na mgonjwa amepona wala hahitaji kutumia mkongojo tena”.

Akakumbusha kuwa: “Teknolojia ya Nadhuur haihitaji kupasua sehemu kubwa ya muili wa mgonjwa, hutoboa sehemu isiyo zidi sentimita moja kwa ajili ya kuingiza kifaa hicho na kwenda kukata sehemu inayo hitajika”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa daima chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magojwa tofauti kila baada ya muda fulani, sambamba na kupokea wagonjwa mbalimbali walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: