Atabatu Alawiyya tukufu: Hakika walioitikia fatwa ya kujilinda ya wajibu kifaya walikwenda kwenye uwanja wa vita sio kwa tamaa ya mali wala kugombania madaraka

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu kupitia mjumbe wa kamati kuu yake na rais wa kitengo cha habari Ustadh Faaiqi Shimri amesema kuwa: Hakika walio itikia fatwa ya kujilinda ya wajibu kifaya, walikwenda kwenye uwanja wa vita sio kwa tamaa ya mali wala kugombania madaraka, msimamo wao haukuchanganyika na mambo mengine ya tamaa za dunia, mmebakia katika msimamo wenu wa kulinda taifa, msichafuliwe na wajinga, endeleeni na msimamo wenu mtukufu, mtapata mbele ya Mwenyezi Mungu mambo makubwa yasiyo lingana na mambo ya duniani.

Hayo yamesemwa katika ujumbe wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la Hashu-Atabaat linalo simamiwa na viongozi wa kikosi cha Imamu Ali (a.s), kikosi cha Ali Akbaru (a.s), kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Answaru Marjaiyya, kongamano ambalo limeanza leo Jumanne mwezi (15 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (1 Desemba 2020m) katika Atabatu Alawiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Hashdu-Atabaat walinzi wa fatwa na wajenzi wa taifa).

Shimri akabainisha kuwa: “Siwezi kuongea mengi mbele ya nyuso hizi tukufu ispokua kuwaambia karibuni sana ndugu zangu mujahidina watukufu watu mliojitolea kuilinga Iraq kwa gharama ya roho zenu katika kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye bariki taifa hili kwa fatwa ya kujilinda ya jihadi kifaya, ikawa fimbo iliyokimbiza nyoka wakali na kuwazuwia wasivunje heshima ya taifa na kuchafua maeneo matakatifu”.

Akaendelea kusema: “Enyi majemedari, mmethibitisha kuwa kumuamini Mwenyezi Mungu ni siraha kubwa iliyotunzwa ndani ya vifua vyetu, hakuna mwenye shaka, hakika hatukusukumwa na kitu chochote zaidi ya Imani iliyojaa katika vifua vyetu, tukatoka kutafuta ushindi au shahada, tukamshinda shetani na kuharibu mikakati yake, akakimbia katika uwanja wa vita”.

Naam, Imani hiyo inatokana na kumpenda Ali (a.s) kwa dhati katika nafsi zetu, pamoja na kufanya ibada na zuhudi wakati wa amani, na inakua utoaji na ukarimu wakati wa shida, na huwa ni hasira wakati wa vita, ardhi hii inahuishwa kwa kufanya ibada, ukweli na damu, ni urithi na mazingatio kwa vizazi vijavyo, mti huu uendelee kutoa kivuli cha amani na ukarimu”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awarehemu mashahidi wetu, awape subira na utulivu familia zao, awaponye haraka majeruhi, na atupe amani na utulivu katika taifa letu la Iraq, hakika yeye ni mwingi wa kusikia na mwingi wa kujibu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: