Kuanza ratiba ya kongamano la kwanza la Hashdu Atabaat tukufu

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumanne mwezi (15 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (1 Desemba 2020m) limeanza kongamano la Hashdu Atabaat katika Atabatu Alawiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo (Hashdu Atabaat ni walinzi wa fatwa na wajenzi wa taifa), linalo simamiwa na viongozi wa kikosi cha Imamu Ali (a.s), kikosi cha Ali Akbaru (a.s), kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Answaru Marjaiyya, na kuhudhuriwa viongozi wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Najafu Ashrafu na Karbala, pamoja na wawakilishi wa ofisi za Maraajii-Dini watukufu na viongozi wa Dini bila kusahau ugeni unao wakilisha Atabatu (Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya).

Hafla ya ufunguzi imeanza kwa Quráni tukufu iliyosomwa na Haani Mussawi na kufuatiwa na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa la Iraq.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Alawiyya ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati kuu ya Ataba hiyo na rais wa kitengo cha habari, Ustadh Faaiqi Shimri ambae amesisitiza kuwa: “Hakika walio itikia wito wa fatwa ya kujilinda ya faradhi kifaya, walikwenda kwenye uwanja wa vita sio kwa tamaa ya mali wala kugombania madaraka, jihadi yao haikuchanganyika na mambo mengine ya tamaa za dunia, na mmebakia katika msingi wenu wa kulinda taifa, wala hamjaharibiwa na maneno ya wajinga, endeleeni kubakia katika msimamo wenu wa kulinda taifa na maeneo matakatifu, ili muweze kupata thawabu za Mwenyezi Mungu aliyetukuka ambazo haziwezi kufananishwa na malipo ya duniani”.

Baada yake ukafuata ujumbe wa Ustadh wa Hauza Sayyid Muhammad Ali Baharul-Uluum, akafafanua kuwa: “Hakika Marjaa wetu Mkuu katika khuduba zake zote amekuwa akisisitiza maslahi ya umma wa Iraq na ulazima wa kuwalinda raia wake bila ubaguzi wa kimadhehebu, kidini na kijamii”.

Halafu ikawekwa filamu iliyo onyesha baadhi ya matukio ya vita dhidi ya genge la kigaidi la Daesh iliyo ongozwa na majemedari hawa. Kisha akazungumza muwakilishi wa rais wa jamhuri katika mambo ya ulinzi na usalama Ustadh Najahu Shimri, ambae ameongea kwa niaba ya wizara ya ulinzi, akasema kuwa:

Katika safari ya maisha na matukio makubwa ya kihistoria, unatokeza uzalendo wa taifa na kulinda uhai wa raia na misingi ya maisha kwa kuingia kwenye jihadi ya kulinda umoja wa taifa na maeneo matakatifu, yote hayo yanaongozwa na hisia. Hivyo ndio walivyo Hashdu-Shaábi kwa ujumla, walio anzishwa kutokana na fatwa ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani aliyotoa Juni (2014) ya kujilinda faradhi kifaya, iliyo pelekea kubadilisha muelekeo wa vita na kuleta ushindi kwa taifa na raia wake.

Ujumbe wa mwisho ukatoka kwa Hashdu-Atabaat, uliowasilishwa na Shekh Mikdadi Hamudi Kaabi makamo wa kiongozi mkuu wa kikosi cha Imamu Ali (a.s), akasema kuwa: “Hakika ushindi mkubwa dhidi ya magaidi walio vamia taifa la Iraq, ambao watu wengi walidhani usinge patikana, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na matunda ya fatwa tukufu ya kujilinda ya wajibu kifaya iliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu ulipatikana, na kuongeza hamasa kwa wapiganaji sambamba na kuwapa misaada mbalimbali”.

Kongamano litaendelea tena jioni na kutakuwa na mambo ya kiutawala yatakayo ongozwa na kitengo cha idara ya mali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: