Vikao bado vinaendelea katika kongamano la Hashdu Atabaat la kwanza

Maoni katika picha
miongoni mwa ratiba ya siku ya pili ya kongamano la Hashdu Atabaat la kwanza, linalofanywa na viongozi wa kikosi cha Imamu Ali (a.s), kikosi cha Ali Akbaru (a.s), kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Answarul-Marjaiyya, chini ya kauli mbiu isemayo: (Hashdu Atabaat walinzi wa fatwa na wajenzi wa taifa), asubuhi ya Jumatano, mwezi (16 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (2 Desemba 2020m) vimefanyika vikao kadhaa.

Vikao hivyo ni sehemu ya ratiba ya asubuhi katika siku ya pili ya kongamano, jumla ya vikao vitano vimefanywa na mada mbalimbali zimejadiliwa.

Vikao hivyo vimefanyika katika jengo la Sayyid Shuhadaa (a.s) chini ya Atabatu Husseiniyya, na jengo la Imamu Haadi (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya, pamoja na ukumbi wa Sayyid Auswiyaa (a.s) katika Atabatu Husseiniyya.

Msemaji wa kongamano hili Ustadh Hazim Fadhili ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Vikao vilikuwa na mada tofauti zilizo wasilishwa leo asubuhi, kulikuwa na mada inayo husu utowaji wa mafunzo katika vikosi hivyo vinne, na mada kuhusu utendaji wa vitengo vya chakula pamoja na mada kuhusu utendaji wa vitendo vya sheria”.

Akaongeza kuwa: “Pia kulikuwa na mada ya kujadili vitengo vya upelelezi na usalama, pamoja na vitengo vya mahusiano”.

Akaendelea kusema: “Tutakusanya maoni yote yaliyo tolewa kwenye vikao hivyo na kuyawasilisha kwa wahusika, kwa ajili ya kuyafanyia kazi na kuboresha utendaji wa vikosi hivyo”.

Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Ustadh Maitham Zaidi amesema kuwa: “Leo tumejadili mambo matano tofauti, tunatarajia kutoka na maazimio yatakayo kabidhiwa kwa wahusika, ili yasaidie kutatua baadhi ya changamoto na kuboresha utendaji”.

Tambua kuwa kongamano hili limeanza asubuhi ya jana siku ya Jumanne katika Atabatu Alawiyya tukufu, na kuhudhuriwa na viongozi wa ulinzi na usalama kutoka mkoa wa Najafu na Karbala, pamoja na wawakilishi kutoka ofisi za Maraajii Dini watukufu, na viongozi wa Dini kutoka hauza, bila kusahau wageni maalum walio wakilisha Atabatu (Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: