Makongamano na matamasha ni matukio matukufu katika Ataba takatifu

Maoni katika picha: picha zilizopo (sehemu ya shug
Kituo cha elimu na ubunifu chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu huchukuliwa kuwa ni kituo muhimu cha utamaduni, kina ofisi nyingi zilizo chini yake, miongoni mwa ofisi hizo ni hii ya makongamano na matamasha, ambayo ndio kiunganishi kikuu cha kitamaduni na kielimu, kwa kuandaa kuratibu na kuendesha makongamano, matamasha, nadwa na mikutano ya ndani na ya nje.

Ustadh Ridhwani Salaami mkuu wa kituo hiki ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika hii ni miongoni mwa idara muhimu na inashughuli nyingi, shughuli zake sio zile zinazo fungamana na kituo peke yake au zile zilizo chini ya kitengo cha habari na utamaduni tu, bali kinashiriki kwenye asilimia kubwa ya shughuli zote zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuweka mazingira yanayo endana na utamaduni bora wa kiislamu, ili kuongeza uwelewa kwenye mambo tofauti”.

Akabainisha kuwa: Idara hii huandaa na kusimamia makongamano ya kimataifa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na nadwa na mikutano ya kielimu na kitamaduni, miongoni mwa makongamano muhimu ni: (Hema la Ashuraa nchini Uturuki na kongamano la kiongozi wa waumini –a.s- nchini India) na mengineyo.

Kiongozi wa idara ya makongamano na matamasha Uastadh Ali Mahadi amesema kuwa: “Makongamano na matamasha ni sehemu ya mawasiliano ya kifikra na kitamaduni baina ya jamii tofauti, Atabatu Abbasiyya inalipa umuhimu mkubwa swala hilo, ndio maana kuna idara maalum inayo husika na kuratibu shughuli hizo ndani na nje ya Ataba tukufu”.

Akabainisha kuwa: Idara inawatumishi wenye uzowefu mkubwa wa kuendesha makongamano na matamasha ya kimataifa na kitaifa, pamoja na shughuli zingine zinazo toa picha halisi ya Ataba takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: