Hashdu Atabaat tukufu: Tunaendelea na mwenendo wetu wa kulinda amani na utulivu wa taifa pamoja na kulinda heshima ya taifa

Maoni katika picha: sehemu ya kikao
Wawakilishi wa vikosi vya Hashdu Atabaat, kikosi cha Imamu Ali (a.s), Abbasi (a.s), Ali Akbaru (a.s) na Answaru Marjaiyya, wamesema kuwa tunaendelea na mwenendo wetu wa kulinda amani na utulivu wa taifa pamoja na heshima yake.

Yamesemwa hayo kwenye kikao kilicho fanywa asubuhi ya Alkhamisi mwezi (17 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (3 Desemba 2020m) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambacho kilikuwa sehemu ya vikao vya mwisho wa kongamano lililodumu kwa muda wa siku tatu, kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa kongamano la Hashdu Atabaat Ustadh Hazim Fadhili aliyo toa kwa mtandao wa Alkafeel, amesema kuwa: “Mambo mengi tumeongea ambayo ni sehemu ya kukamilisha yale tuliyojadili siku mbili za nyuma, yanayo lenga kupata msimamo wa pamoja katika kuboresha mambo ya kiutawala na kimali kwenye vikosi hivyo”.

Akaongeza kuwa: “Katika kikao hicho tumejadili pia mambo yaliyo kubaliwa katika vikao vilivyo tangulia, na kuandika maazimio ya kongamano yaliyoangazia mambo tofauti, kikoa hiki ndio kilicho chambua mambo kwa kina na kubaini mahitaji, pamoja na kusisitiza ulazima wa kushikamana na malengo ya kuanzishwa kwa vikosi hivi, kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa la Iraq na heshima yake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: