Muhimu.. Maazimio ya kongamano la Hashdu Atabaat la kwanza

Maoni katika picha
Washiriki wa kongamano la Hashdu Atabaat la kwanza linalo simamiwa na viongozi wa kikosi cha Imamu Ali (a.s), Abbasi (a.s), Ali Akbaru (a.s) na Answaru Marjaiyya, chini ya kauli mbiu isemayo: (Hashdu Atabaat walinzi wa fatwa na wajenzi wa taifa), ambalo kikao chake cha mwisho kimefanywa Alasiri ya leo siku ya Alkhamisi mwezi (17 Rabiul-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (3 Desemba 2020m) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wametoa maazimio na maoni kutokana na mambo waliyo jadili ndani ya muda wa saa sabini na mbili zilizo pita, maazimio hayo yamesomwa na rais wa kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Mushtaqu Abbasi Muan, kama ifuatavyo:

Kwanza: Kutokana na uvunjifu wa amani uliotokea hivi karibuni na kuendelea kuwepo kwa mambo yanayotishia amani ya taifa na raia, vikosi vya Hashdu Atabaat ambavyo vilikuwa, vinaendelea, na vitaendelea kuwa mlinzi wa uhakika wa taifa kipenzi na raia wake, viko tayali kuendelea kulinda fatwa na kutekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Sistani, Mwenyezi Mungu awaneemeshe wairaqi na wengineo kwa kurefusha umri wake mtukufu, tunasisitiza kuwa sisi ni walinzi wa taifa la Iraq na amani ya wananchi wake pamoja na maeneo matakatifu, tunapambana na kila anaetaka kuharibu amani na utulivu wa taifa hili, jambo hilo limethibitishwa na vikosi vyetu siku za nyuma katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh, na tunarudia kusisitiza utayali wetu kupitia kongamano hili.

Pili: Hakika kulinda ushindi uliopatikana katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh ndio kipaombele cha kwanza kwetu, sambamba na kulinda heshima ya jihadi na wanajihadi, na kuwasafisha na kila uchafu wanaopakwa, jambo hilo limefanywa na vikosi vyetu wakati wote wa vita ya kukomboa miji, jambo lililo pelekea wananchi kuwataka wapiganaji wetu waendelee kubaki katika maeneo yao baada ya kuwaondoa magaidi wa Daesh, aidha jambo hilo limekuza ushirikiano na jamii ya raia wa taifa letu tukufu.

Tatu: Hakika Hashdu Atabaat tukufu wanasisitiza kuheshimu sheria na katiba ya Iraq, na kuzuwia wapiganaji wake kufanya jambo lolote linalohalifu sheria na katiba ya nchi, ikiwa ni pamoja na kujiingiza matika mambo ya siasa, ushabiki wa vyama vya siasa, aidha tunatoa uhuru wa kushiriki kwenye uchaguzi wapiganaji wetu kama wapiga kura na sio wagombea, pamoja na kusaidia kupiga vita ufisadi bila kuingilia malumbano ya kisiasa, tunatekeleza majukumu yetu kwa umakini na uaminifu mkubwa.

Nne: Hashdu Atabaat tunasisitiza kuwa ujenzi wa taifa na mustakbali wake, pamoja na kulinda historia yake unaanzia kwenye kupiga vita ufisadi ambao ni msingi wa kupora haki za raia na tunu zao, na kuzuwia nguvu kazi kujenga taifa na kuhudumia raia, wafanyakazi wa umma wanatakiwa kujua hatari na ubaya wa ufisadi.

Tano: Hakika Hashdu Atabaat ambayo ipo chini ya amirijeshi mkuu kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na waziri mkuu wa zamani, inasubiri serikali itekeleze makubaliano hayo ili tuanze kutekeleza wajibu wetu kitaifa, kuchelewa kufanyiwa kazi makubaliano hayo kuna athari ya moja kwa moja katika utekelezaji ya majukumu ya wapiganaji, na kunachelewesha miradi ya kibinaadamu ambayo inafanywa na wapiganaji hao pamoja na matatizo mengine yanayo weza kujitokeza.

Sita: Tunataka mamlaka zinazo husika za bunge na serikali, kulipa umuhimu swala la kuwa na idara inayo jitegemea ya wapiganaji wa Hashdu Shaábi itakayo shughulikia haki zao, pamoja na kuangalia daraja zao na wapewe stahiki zao sawa na askari wengine wa serikali, hiyo ni sehemu ndogo ya kuwajibika kwao kutokana na namna walivyo jitolea kwa ajili ya taifa lao.

Saba: Pia tunaomba mamlaka zinazo husika kufuata maelekezo ya mahakama ya kumpa uhuru askari wa kuchagua sehemu ya kuchukulia mshahara wake, na sio kuwalazimisha kwenda kuchukua sehemu maalum kama ilivyo sasa, kufanya hivyo kutatoa nafasi ya ushindani kwa mashirika, jambo hili tumesha liomba kwa wahusika na hatujapata majibu yeyote hadi sasa.

Nane: Familia za mashahidi na majeruhi wanahaki ya kuishi katika nyumba nzuri za serikali chini ya miradi mbalimbali inayo fanywa na serikali.

Mwenyezi Mungu aihami nchi yetu kipenzi na Maraajii wetu watukufu pamoja na wapiganaji wetu imara, rehema za milele ziwepamoja na mashahidi watukufu na wagonjwa na majeruhi wapone haraka, na amani iwe juu yenu pamoja na baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: