Kongamano la kitamaduni Multaqal-Qamaru limehitimisha ratiba yake kwa vijana wa Muthanna

Maoni katika picha
Kituo cha kongamano la kitamaduni Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimemaliza ratiba yake kwa vijana wa wilaya ya Ramitha na miji mingine ya mkoa wa Muthanna, chini ya utaratibu wake unaolenga kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni na kijamii, kwa kutumia elimu za kisasa, wala sio kwa kutumia chuki na mizozo ambayo huwa na matokeo mabaya katika jamii.

Shekh Haarith Dahi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “hakika kongamano hili ni sehemu ya ratiba za kituo hiki, safari hii tumelenga vijana zaidi ya (35), wameandaliwa ratiba ya siku tano, wamefundishwa mambo tofauti, yakiwemo mambo ya Dini, historia na uzalendo”.

Akaongeza kuwa: “Tumejadili mazingira halisi ya vijana na njia za kuwaendeleza ili kunufaika nao kutokana na mafundisho ya Ahlulbait (a.s) sambamba na kuyafanyia kazi”.

Kumbuka kuwa mara nyingi baada ya vijana kupewa mafunzo ya (Multaqal-Qamaru) katika miji yao hupewa semina, wasimamizi wanasema kuwa program ya (Multaqal-Qamaru) inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, inamchango mkubwa katika kuandaa vijana waweze kubeba majukumu ya kidini, kijamii na kitaifa, kwa kupambana katika vita ya kifikra isiyo isha kama inavyo isha vita ya kijeshi, Ataba tukufu imegharamia kila kitu kuanzia uandaaji wa ratiba hadi wahadhiri, usafiri, malazi, chakula na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: