Toleo la nakala ya saba katika program ya (kitabu changu thamani yangu)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa nakala ya saba katika program ya (kitabu changu thamani yangu) inayo lenga wasichana wa umri tofauti, nakala hii ni muendelezo wa nakala za mwaka jana, na kutilia msisitizo mafanikio yake.

Mkuu wa kituo hicho bibi Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Program hii ni kwa ajili ya kuongeza uwezo wa mwanamke na kumshughulisha katika faragha zake kwa mambo yenye manufaa kwake, kutokana na wingi wa washiriki pamoja na hamasa ya kutaka kushiriki katika program hii tumeweza kuendelea kutoa nakala hadi tumefika kwenye nakala hii”.

Akaongeza kuwa: “Program hii inakusudia kuamsha hamasa ya kujifunza utamaduni na mambo mengine ili kuhakikisha mwanamke anatumia muda wake katika mambo yenye faida kwake duniani na akhera, pamoja na kumjengea kujiamini na kuwa na uwelewa salama”.

Akabainisha kuwa: “Muda wa kushiriki kwenye program hii ni suku (15), mshiriki huulizwa maswali yanayo saidia kujua kiwango cha elimu yake na uwezo wake pamoja na maisha yake ya kila siku, mwisho wa awamu hii na baada ya kupigiwa kura majibu sahihi watatangazwa washindi watatu”.

Kushiriki katika program hii jiunge kupitia link ifuatayo https://forms.gle/grKSC1aSuLNdniDr8
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: