Mkuu wa chuo cha Imamu Alkaadhim: Chuo kikuu cha Alkafeel kinauzowefu mkubwa katika sekta ya elimu ya juu hapa Iraq

Maoni katika picha
Kiongozi wa chuo cha Imamu Alkaadhim (a.s) Dokta Ghina Khaqani amesema kuwa, chuo kikuu cha Alkafeel kinauzowefu mkubwa katika sekta ya elimu ya juu hapa Iraq, kina vifaa vya kisasa katika kila anacho hitaji mwanafunzi na mwalimu darasani vinavyo afikiana na mazingira ya chuo, tunataraji kufungua milango ya ushirikiano kwa faida ya pande zote mbili.

Yamesemwa hayo baada ya ziara iliyofanywa na Khaqani mbele ya wenyeji wake ambao asilimia kubwa walikua ni marais wa vitengo vya chuo, katika chuo kikuu cha Alkafeel ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kikao hicho kilihudhuriwa pia, na rais wa kamati na mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, chini ya wenyeji wa rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuris Dahani.

Wageni wametembelea kumbi za madarasa na maabara pamoja na majengo ya chuo kwa ujumla, sambamba na kuangalia vifaa vya kufundishia, rais wa chuo alitoa ufafanuzi kuhusu kila kitu walicho ona katika ziara hiyo ya kielimu.

Msaidizi wa mkuu wa taaluma katika chuo hicho Dokta Muhammad Waadhwihi amesema kuwa: “Hakika kazi nzuri na kubwa imefanywa katika sekta ya majengo na elimu, mazingira ya usomaji ni mazuri, jambo hili linatusukuma kujenga ushirikiano katika sekta ya elimu na utafiti”.

Baada ya ziara hiyo wageni wakaushukuru uongozi wa chuo kikuu cha Alkafeel kwa kuwapa mapokezi mazuri, na wakasema wanatarajia kufanya ziara kama hiyo siku zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: