Kituo cha turathi za Najafu Ashrafu kimemaliza semina ya (Juud Alkafeel) ya faharasi, iliyo fanywa na kituo cha turathi za kusini kwa kushirikiana na kituo cha turathi za Najafu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kupewa somo la namna ya kuhakiki faharasi za nakala-kale ndani ya siku saba, iliyo wasilishwa na mhakiki Ustadh Ahmadi Ali Majidi Alhilli.
Alhilli amebainisha kuwa: “Semina hii imefanywa chini ya utaratibu wa kushirikiana kielimu na kimaarifa kati ya vituo na idara zilizo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kutoa fani hii kwa watu wanao hitaji”.
Akaongeza kuwa: “Katika semina hii wamefundishwa masomo ya faharasi za nakala-kale ambayo ni masomo nadra hapa Iraq, zimewasilishwa mada nzuri zinazo muwezesha mhakiki kupata mambo mengi kuhusu nakala-kale, ukizingatia kuwa nakala-kale hutambulisha turathi na historia ya umma na mataifa tofauti na watu wa dini tofauti na mila mbalimbali, fani ya faharasi na uhakiki ni sawa na kioo kinacho onyesha nakala-kale na elimu yake pamoja na mila zake, mtu anapo taka kufanya uhakiki lazima awe na elimu ya kutosha ya namna ya kufanya uhakiki, bila kuangalia faharasi na nakala-kale hawezi kufahamu kuna nakala ngapi za kitabu hicho, kama zipo nyingi zingine ziko wapi, kama nakala aliyo nayo sio sahihi ikowapi nakala sahihi, kama ikiwa nyeusi ikowapi nyeupe”.
Tambua kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kikomstari wa mbele daima katika kutoa semina na mihadhara, kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wake, nacho ni kitengo maalum cha kuhuisha turathi za kiislamu na kufichua hazina zilizo jifisha, ambazo ni turathi za kihistoria zilizo jificha katika nakala-kale.