Chuo kikuu cha Al-Ameed katika mfumo wa kimataifa (Green Metric)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeigia katika vyuo vinavyo ingia katika mpango wa kimataifa wa maendeleo endelevu katika mwaka wa 2020m, na kuwa chuo cha (770) duniani katika katika mfumo wa (Green Metric) na kimekua chuo cha (29) katika vyuo vya serikali na binafsi vya hapa Iraq.

Serikali kupitia wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu ilikuwa imeshaweka utaratibu wa kuingia vyuo vikuu vya Iraq katika mfumo wa kimataifa kama ishara ya kuwa na mfumo bora wa elimu hapa Iraq, kutokana na mpango huo ndio chuo kikuu cha Al-Ameed kikaanza kujiandaa kuingia kwenye mfumo huo.

Rais wa chuo cha Al-Ameed Dokta Muayyad Imrani Alghazali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika chuo kikuu cha Al-Ameed kimefuata utaratibu wa wizara kuingia katika mfumo wa kimataifa, tumekamilisha vigezo ndani ya muda mfupi na tumeingia katika kundi la vyuo (61) vilivyopo katika mfumo wa (Green metrics) miongoni mwa vyo vya serikali na binafsi”.

Akasisitiza kuwa: “Chuo kiliweka mkakati wa kuingia kwenye mfumo wa kimataifa, hivyo kikaweka mkakati wa kutimiza vigezo na masharti yaliyo wekwa, ikiwa ni pamoja na kutilia umuhimu tafiti za kielimu kwa ajili ya kuingia kwenye mfumo huo, jambo hilo lina nafasi kubwa kwenye vigezo vyote, ikaundwa kamati ya kufuatilia mpango wa kuingia katika mfumo wa kimataifa, jukumu lake kubwa likawa ni kutekeleza vigezo vya kuingia kwenye mfumo huo”.

Kumbuka kuwa mfumo wa (Green Metric) unalenga kupima utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu kwenye vyuo vikuu dunia nzima, chini ya kifungu cha (76) kinacho husu mpangilio wa vyo vikuu kwa kuangalia mkoa na mazingira ya chuo, vyuo vingi duniani vimeingizwa kwenye mfumo huo, huu ndio mfumo wa kwanza kimataifa uliopo chini ya malengo ya maendeleo endelevu, kwani umejikita katika utunzaji wa mazingira.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: