Idara ya uhusiano wa vyuo inatoa pongezi kwa wahitimu wa chuo cha Kufa

Maoni katika picha
Idara ya uhusiano wa vyuo na shule chini ya kitengo kikuu cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, inatoa pongezi kwa wahitimu wa chuo cha Kufa wa mwaka wa masomo (2019 – 2020).

Kiongozi wa idara ya mahusiano katika idara hiyo Ustadh Muntadhir Swafi amesema kuwa: “Wanafunzi hawa wamekuja kula kiapo cha kuhitimu mbele ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Tumewapokea chini ya ratiba ya elimu na utamaduni iliyo pangwa na idara yetu kwa wanafunzi wa chuo kwa ujumla, kutokana na umuhimu wa watu hawa na nafasi yao katika kujenga taifa”.

Akaendelea kusema: “Tumeandaa ratiba kamili ya wanafunzi wageni, inayo husisha kufanya ziara katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na kutembelea vitengo vyake na baadhi ya maeneo yake”.

Akabainisha kuwa: “Tumehitimisha ratiba kwa kuwapa zawadi wanafunzi hao, pamoja na kuwapa mawaidha elekezi yaliyo tolewa na Sayyid Muhammad Mussawi kiongozi wa idara ya maelekezo ya kidini katika kitengo cha Dini, halafu wakaangalia filam ya (Sayyid Al-Maa) pamoja na filamu inayo onyesha miradi mikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, halafu wakapewa vyeti vya ushiriki kwenye ratiba hii”.

Wanafunzi wametoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia idara ya uhusiano wa vyuo vikuu na shule kwa mapokezi mazuri waliyo pewa, wakasema kuwa hili sio jambo geni kufanywa na Ataba tukufu, kwani imekua mstari wa mbele daima katika kusaidia wanafunzi wa vyuo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: