Waziri wa utamaduni amesema kuwa: Chuo kikuu cha Alkafeel kimeonyesha thamani ya elimu kwa kuandaa mazingira bora kwa mwalimu na mwanafunzi

Maoni katika picha
Waziri wa utamaduni na utalii Dokta Hassan Naadhim amesema kuwa: chuo kikuu cha Alkafeel kinathamini elimu sana, kimeweka mazingira mazuri ya mwanafunzi na mwalimu, kwa ajili ya kuboresha elimu hapa nchini, jambo hili linapendeza na kufurahisha.

Yamesemwa hayo alipotembelea chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kupokewa na jopo la wajumbe wa kamati ya uongozi, akiwemo rais wa kamati ya walimu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi na mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel pamoja na rais wa kitengo cha habari za Ataba takatifu, wakiambatana na Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani rais wa chuo, aliyekuwa anawafafanua mambo yaliyopo katika chuo, kuanzia kumbi za madarasa, maabara na nyumba za chini, sambamba na kueleza mikakati ya baadae.

Waziri akasema: “Ni vizuri mwanafunzi wa Iraq akapata chuo bora kama hiki, kinatekeleza kwa kiwango cha juu kanuni zoto za vyuo binafsi, mimi nimekua nikifuatilia utendaji wake tangu siku ya kwanza niliyo ingia katika wizara ya elimu ya juu, natarajia wataendelea kufanya vivuri na kuwa chuo bora zaidi hapa Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: