Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limepata mwitikio mkubwa katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa hapa Iraq.

Maoni katika picha
Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linaloshiriki kwenye maonyesho ya kimataifa ya vitabu hapa Iraq, limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya, limekua kivutio kikubwa kwao kutokana na aina ya vitabu walivyo navyo kuwa vinakidhi mahitaji yao kifikra na kitamaduni kwa watu wa rika zote.

Haya yamesemwa na kiongozi wa maonyesho Sayyid Muhammad Aáraji, akaongeza kuwa: “Pamoja na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya changamoto ya janga la Korona, raia wa Iraq wanajali mambo ya elimu na utamaduni, maonyesho ya Iraq yamefana pamoja na mazingira hayo, tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu iliyo wakilishwa na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu ya kibinaadamu, tangu siku za kwanza zimeshuhudia watu wengi wakija kutembelea meza yao, kwa ajili ya kuangalia, kununua au kuuliza maswali kuhusu Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa sababu za kuvutia watu, tawi letu ni tofauti na matawi mengine ya kitaifa na kimataifa, machapisho yaliyopo katika tawi hili ya kifikra, kitamaduni, kihistoria, turathi, dini na mengine, hayapatikani katika tawi lingine lolote, kwa sababu machapisho yetu ni kazi ya Ataba tukufu kuanzia kuandika, kuhakiki na kuchapisha, hiyo ndio sifa ya pekee katika ushiriki wetu”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi kwenye maonyesho ya kimataifa ambayo hufanywa Bagdad na ambayo ni muhimu kwake, sambamba na kushiriki kwenye maonyesho kama hayo ndani na nje ya Iraq, yanayo endana na malengo yake ya kusambaza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), na hushuhudia ongezeko la watu wanao tembelea banda lao kwenye kila maonyesho, kutokana na kuwa kwake na ongezeko la machapisho mapywa kwenye kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: