Kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi kimepokea wageni kutoka kituo cha turathi za Basra kwa ajili ya kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja

Maoni katika picha
Kituo cha upigaji picha wa nakala-kale na faharasi chini ya maktaba na daru makhtutwaat katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepokea ugeni kutoka kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, katika kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja sambamba na kuweka mipango ya pamoja kuhusu turathi, nakala-kale na shuhuda za kihistoria.

Ugeni huo ukiongozwa na makamo mkuu wa kituo Shekh Yasini Yusufu umetembelea maeneo ya kituo na kuangalia mfumo wake kielimu na kumpangilio, wakasikiliza maelezo kuhusu utendaji kwenye sekta ya turathi na nakala-kale na mambo ya kihistoria, ikiwa ni pamoja na faharasi, uchambuzi, upigaji wa picha, na utunzaji wa aina adimu za karatasi, mambo ambayo yanawakilisha historia ya nakala-kale kwa ujumla, wameangalia pia maktaba maalum ya faharasi na nakala-kale.

Mkuu wa kituo cha upigaji picha wa nakala-kale na faharasi Ustadh Swalahu Siraji ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu ziara hiyo, kwa kusema kuwa: “Katika kuendeleza ushirikiano wetu, tumetembelewa na wageni kutoka kituo cha turathi za Basra waliokuja kuangalia utendaji wa kituo chetu, na kutambua vitengo vyake na mafanikio yake katika sekta ya turahi”.

Akafafanua kuwa: “Tangu kuanzishwa kwa kituo hiki tumekuwa tukijali sana kushirikiana na vituo vya turathi kila sehemu ya Iraq na ulimwengu wa kiarabu na kiislamu kwa ujumla, tunaunganishwa na lengo moja kubwa ambalo ni kulinda na kutunza vielelezo vya kihistoria, tumepata ushirikiano kubwa kutoka kwenye vituo vya turathi”.

Kumbuka kuwa kituo cha upigaji picha wa nakala-kale na faharasi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinajukumu la kufanyia kazi vielelezo vya kihistoria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kimepata mafanikio makubwa katika sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: