Kuendesha opresheni ya kupambana na magonjwa ya mitende katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Idara ya upandaji miti ya mapambo chini ya kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, imeanza opresheni iitwayo kupambana na maradhi ya miti ya mitende iliyopo katika eneo hilo takatifu, ili kuzuwia maradhi ambayo huifanya isikue vivuri.

Kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Haatim Abdulkariim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Miti ya mitende ni moja ya kivutio muhimu katika eneo hilo, idara inaipa kipaombele zaidi na kuilinda na aina zote za maradhi ya miti, hii ni moja ya shughuli nyingi ambazo hufanywa katika miti hiyo, ikiwa ni pamoja na kuisafishia, kuichambulia, kuisamadia na zinginezo, ilimradi iwe katika hali nzuri”.

Akaongeza kuwa: “Opresheni hii imehusisha kupuliza dawa ya kuuwa bakteria wanao sababisha maradhi kwenye mitende, dawa hii hupulizwa katika msimu kama huu, tumetumia dawa nzuri na rafiki kwa mazingira, haina madhara yeyote kwa mazuwaru na watu wanaopita eneo hilo, kazi hii itaendelea kwa siku kadhaa hadi tutakapo maliza kupuliza kwenye miti tote iliyopo eneo hili”.

Kumbuka kuwa mitende iliyopandwa katika eneo la katikati ya haram mbili huchukuliwa kuwa moja ya miti muhimu, pamoja na umaalum wake katika eneo hilo, kuna mitende (57) kama ishara ya umri wa Imamu Hussein (a.s) siku aliyo uwawa katika ardhi hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: