Kugawa misaada ya chakula katika mitaa ya mafakiri mjini Karbala

Maoni katika picha
Kamati ya maelekezo na misaada chini ya kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha ratiba ya kugawa unga kwa familia zinazo ishi kwenye mitaa ya mafakiri ndani ya mkoa wa Karbala, kupitia mradi wa (Marjaiyyatu-Takaaful) unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kama sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa opresheni hiyo Shekh Haidari Aaridhwi amesema kuwa: “Opresheni hii ni muendelezo wa opresheni zingine nyingi zilizo fanywa tangu ilipotolewa fatwa ya kusaidiana na Marjaa Dini mkuu, iliyo himiza kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kuathiriwa na mazingira ya janga la Korona, ili kuwapunguzia ugumu wa maisha japo kidogo”.

Akasisitiza kuwa: “Hivi ndio inavyo takiwa sawa iwe misaada hiyo inatolewa na Atabatu Abbasiyya au na watu wengine, ni jambo ambalo linaonyesha uponde wa Mwenyezi Mungu na juhudi ya kuondoa balaa na kuwa na mwisho mwema, hii misaada midogo inayo gawiwa inasaidia kupunguza shida katika familia hizo”.

Kumbuka kuwa kitengo cha Dini kutokana na uwezo kilio nao, kilianza kutoa misaada tangu siku za kwanza lilipo tangazwa janga la virusi vya Korona na kupiga marufuku ya kutembea, kilizitafuta familia za mafakiri na watu walio athiriwa na marufuku hiyo hasa wale ambao riziki zao zinategemea kutoka kila siku, kikaongeza juhudi zaidi baada ya Marjaa Dini mkuu kutoa fatwa ya ulazima wa kusaidia familia za mafakiri na watu walioathiriwa na marufuku ya kutembea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: