Wadau wake: Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Iraq limekua kituo cha zawadi za kiroho na kimaarifa

Maoni katika picha
Watu wanaotembelea tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa hapa Iraq yanayo endelea hivi sasa mjini Bagdad, wamesema kuwa tawi hilo ni kituo muhimu cha zawadi za kiroho na kimaarifa, aidha ni fursa ya kuangalia kazi zinazo fanywa na Ataba tukufu ambazo zinastahiki pongezi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyid Muhammad Aáraji kiongozi wa idara ya maonyesho, na msimamizi wa tawi linalo shiriki kwenye maonyesho haya, linaloundwa na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, akaongeza kuwa: “Watu waliotembelea tawi hilo wameonyesha kuridhishwa na wametuomba tuendelee kushiriki kwenye maonyesho mengine, kwani tulikuwa na machapisho yanayo kidhi mahitaji yao kielimu na kitamaduni, pamoja na upekee wa tawi hili kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akasendelea kusema: “Watu walio tembelea tawi letu hawakutosheka na kuchukua vitabu peke yake, bali waliuliza maswali na kuhitaji ufafanuzi kuhusu miradi ya Atabatu Abbasiyya pamoja na huduma ambazo Ataba imekua ikitoa kwa wananchi wa Iraq”.

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye maonyesho haya ni muendelezo wa ushiriki mwingi wa maonyesho ya aina hii, upekee wa machapisho yetu ni sifa kubwa tuliyo nayo kwenye maonyesho haya, tunazaidi ya machapisho (300) ya aina tofauti, yote ni kazi halisi iliyofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kuanzia uandishi hadi uchapishaji, jambo hili halipatikani kwenye matawi mengine, vitabu tunavyo onyesha vimethibitisha kazi inayo fanywa na Ataba katika sekta ya elimu na utamaduni, kutokana na vitabu vya utamaduni, turathi na elimu tofauti vilivyo andikwa kisasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: