Balozi wa Oman nchini Iraq ametembelea tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu na amesifu machapisho yake.

Maoni katika picha
Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu yanayo fanyika hivi sasa katika mji mkuu wa Bagdad kwenye uwanja wa maonyesho, balozi wa nchi ya kifalme ya Oman Sayyid Haamid bun Aqiil ametembelea maonyesho hayo.

Amefika katika banda la tawi la kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuangalia machapisho waliyo nayo, pamoja na kusikiliza maoelezo kutoka kwa wasimamizi, amesifu ziara hii na kusema ni fahari kwake, machapisho aliyo yaona ni mazuri na amewatakia mafanikio mema wasimamizi.

Tambua kuwa tawi la Atabatu Abbasiyya limepata muitikio mkubwa tangu siku ya kwanza, na limetembelewa na viongozi mbalimbali sambamba na watu wa kawaida, wote wamesifu na kusema kuwa ni mahala pazuri kwa kupata zawadi ya kiroho na kimaarifa.

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye maonyesho haya ni muendelezo wa ushiriki mwingi wa maonyesho ya aina hii, upekee wa machapisho yetu ni sifa kubwa tuliyo nayo kwenye maonyesho haya, tunazaidi ya machapisho (300) ya aina tofauti, yote ni kazi halisi iliyofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kuanzia uandishi hadi uchapishaji, jambo hili halipatikani kwenye matawi mengine, vitabu tunavyo onyesha vimethibitisha kazi inayo fanywa na Ataba katika sekta ya elimu na utamaduni, kutokana na vitabu vya utamaduni, turathi na elimu tofauti vilivyo andikwa kisasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: