Katika wiki ya kimataifa ya fani ya kompyuta: Shule za Al-Ameed zimeanzisha program ya (Saa ratiba) katika shule tatu

Maoni katika picha
Kufuatia wiki ya kimataifa ya fani ya kompyuta, kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza program ya kufundisha (Saa ratiba) katika shule tatu (shule ya wasichana Alqamaru, Nurul-Abbasi na shule ya Al-Ameed).

Rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Ahmadi Swabihi Kaábi amesema kuwa: “Program hii inalenga kuongeza uwezo wa wanafunzi katika fani ya elimu ya Komyuta, na kuongeza maarifa yao katika mambo tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Program hii imeandaliwa kwa ajili ya shule za Al-Ameed na ili kuendana na maendeleo ya ulimwengu, zaidi ya nchi (180) za kiarabu na kiajemi zinatumia program hiyo, jambo hili linaongeza ubora katika shule hizo”.

Ustadh Aárafi Abdulhussein mwalimu wa kompyuta katika shule ya sekondari ya Alqamaru ya wasichana amesema kuwa: “Program ya (saa ratiba) ni program ya kimataifa ambayo hufanyika kwa muda wa wiki nzima katika mwezi wa Desemba kila mwaka, ambapo huwa kuna ratiba maalum ya maswala ya kompyuta”.

Akabainisha kuwa: Tumechagua kipengele cha utambuzi wa kifaa kwa ajili ya kumfundisha mwanafunzi namna ya kuangalia maelezo kwenye kifaa, na namna ya kuongeza taarifa kupitia program hiyo, na kutatua baadhi ya changamoto wanazo pata, kwa mfano kupata taarifa potofu, program hii inasaidia kutambua mambo ya msingi katika kompyuta.

Akasisitiza kuwa: “Tunajitahidi kushirikiana na taasisi zingine siku za mbele kwa ajili ya kuwajengea uwezo zaidi walimu wa shule zetu na kuwafanya wawe na uwezo mkubwa wa kutumia program hiyo, jambo kubwa kwao ni kuwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao”.

Kumbuka kuwa program hii ni sehemu ya teknolojia na elimu za kisasa, na inatoa nafasi ya kunufaika na uwezo wa wataalamu wa kompyuta na lugha ya namba, chini ya selebasi ya masomo ya mwaka (2020/2021m)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: