Multaqal-Qamaru inafanya vikao na vijana kwa kushirikiana na kituo cha utamaduni cha Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya kikao cha vijana kwa kushirikiana na kituo cha utamaduni cha Imamu Hussein (a.s) katika kitongoji cha Mahanawiyya mkoani Baabil, kikao hicho kimelenga wakazi wa mji huo hususan vijana, chini ya ratiba iliyo andaliwa na kituo inayo lenga kujenga uhusiano mzuri na taasisi zingine, na kufanya kazi kwa pamoja katika jamii, kwa kujenga uwezo wa kupambana na changamoto za kijamii.

Mkuu wa kituo cha Multaqal-Qamaru Shekh Haarith Dahi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika uratibu wa vikao hivi ni moja ya harakati za kituo, na vimetengewa muda maalum katika mwaka, kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya Korona, mwaka huu tumepunguza idadi ya vikao hivyo sambamba na kupunguza idadi ya washiriki, aidha tumeandaa wakufunzi wenye uzowefu mkubwa wa kuwasilisha mada zinazojikita katika mahitaji ya raia wa Iraq katika mazingira ya sasa, kikao hiki ambacho kimefanywa katika kitongoji cha Mahanawiyya ni katika muendelezo wa vikao hivyo, na sehemu ya kazi tunazo fanya kwa kushirikiana na vituo vya utamaduni”.

Naye kiongozi wa kikao hicho na mhadhiri Shekh Shawili amesema kuwa: “Kikao chetu cha wiki hii kilikuwa na mada za dini na utamaduni, tulifanikiwa kujibu maswali ya washiriki na kuwapa maarifa ya fikra na maendeleo ya mwanaadamu, na namna ambayo mtu huwa nguzo muhimu na mwenye athari, tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwitikio ulikua mkubwa na majadiliano yalikua mazuri”.

Mkuu wa kituo cha Imamu Hussein (a.s) ameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mradi huu na namna inavyo fuatilia kuhakikisha malengo ya vikao vyake yanafikiwa, na kuwa msingi wa kufanya mambo makubwa zaidi siku zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: