Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya opresheni kubwa ya usafi

Maoni katika picha
Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza opresheni kubwa ya usafi, ambayo ni muendelezo wa shughuli za usafi zilizo fanywa katika barabara za kuingia Karbala upande wa Baabil na Bagdad, kama sehemu ya kusaidia watumishi wa mkoani.

Tumeongea na makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Muhammad Harbi kuhusu opresheni hiyo amesema: “Hakika mradi wa mkanda wa kijani ni muhimu sana katika mkoa wa Karbala, kwani unasaidia kuboresha mazingira ya mkoa na kuufanya uwe na muonekano mzuri, watumishi wetu wameanza kazi ya kufanya usafi na kuondoa takataka kila sehemu”.

Akasema: “Kazi hii itaendelea kwa siku kadhaa, hatua ya kwanza tumesafisha upande wa (Baabil-Karbala) kazi hiyo ilichukua siku saba, baada ya hapo tukahamia katika upande wa (Bagdad – Karbala) kwa muda wa siku saba pia, tumeondoa taka nyingi zilizo kuwa sehemu hizo, sasa hivi tunafanya usafi katika eneo hili muhimu”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya ni sehemu ya ratiba yake na harakati zake kudumisha usafi, mradi huu umejikita upande wa kusini wenye kilometa (27) na ukubwa wa mita za mraba (270,000) inafanya usafi na ukarabati katika eneo hilo, kazi hiyo wamepewa pia kitengo cha shamba boy na kitengo cha usimamizi wa kihandisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: