Shirika la Khairul-Juud limeshiriki katika kongamano la kimataifa kuhusu kilimo

Maoni katika picha
Shirika la kilimo cha kisasa na utengenezaji wa barakoa na vitakasa mikono Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limeshiriki kwenye kongamano la kimataifa kuhusu kilimo, linalo simamiwa na chuo cha uhandisi wa kilimo katika chuo kikuu cha Bagdad chini ya kauli mbiu isemayo: (Utafiti wa kielimu ni msingi muhimu wa kukuza kilimo), wataalamu wa kilimo kotoka ndani na nje ya Iraq wanashiriki kwenye kongamano hilo.

Ushiriki wa kongamano hili umeratibiwa na idara ya mahusiano ya vyuo na shule katika Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa mada zilizo wasilishwa ni mada isemayo: (Utengenezaji wa virutubisho) iliwasilishwa na Ustadh Mhandisi Falahu Abdulhassan katika program ya kulinda mimea na wanyama.

Mambo ya aina mbili yamezungumzwa:

Kwanza: Mambo yanayo husu shirika:

  • - Utambulisho wa shirika.
  • - Vitengo vya shirika.
  • - Bidhaa zinazo tengenezwa na shirika.
  • - Aina za mbolea zinazo tengenezwa na shirika na upekee wake.
  • - Urekebishaji wa ardhi katika viwanda vya shirika.

Pili: Mtaalamu akazungumza kuhusu (bidhaa… aina zake na athari zake) pamoja na kuonyesha bidhaa zinazo tengenezwa na shirika namna zinavyo weza kupambana na maradhi ya mimea.

Mwisho wa mada yake Mhandisi Falahu Abdulhassan Swahibu, akajibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika, naye Dokta Fadhili Hassan Swahafu akasema kuwa: “Hakika ni fahari kubwa kuwa na shirika kama hili hapa Iraq, limesaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha sekta ya kilimo, na bidhaa zake zimechangia kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa chakula kwa raia wa Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: