Atabatu Abbasiyya tukufu imemaliza ushiriki wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa na mkuu wake amesisitiza kuwa yamekua na manufaa

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imekhitimisha ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya kumi, yanayo simamiwa na taasisi ya habari, utamaduni na ufundi, yaliyodumu kwa muda wa siku kumi na kushiriki zaidi ya taasisi za usambazaji (300) kutoka nchi (21) za kiarabu na kiajemi, haya ni maonyesho ya kimataifa ya kwanza kufanywa tangu ilipopigwa marufuku mikusanyiko ya watu kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya Korona.

Mkuu wa maonyesho Ustadh Ihabu Abdurazaaq ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika awamu hii ya maonyesho umekuwa na mafanikio makubwa, tawi lake limepata muitikio mkubwa kutokana na aina ya vitabu vyake, tunatarajia iendelee kushiriki kwenye maonyesho mengine yajayo”.

Kiongozi wa idara ya maonyesho Sayyid Muhammad Aáraji amesema kuwa: Ushiriki wa maonyesho haya ni muendelezo wa ushiriki mwingi wa aina hiyo, jumla ya aina za vitabu zaidi ya (300) vya aina tofauti vimeonyeshwa, vyote vikiwa vimetokana na kazi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kuanzia kuandikwa hadi kuchapishwa, hiyo ndio tofauti kubwa ya tawi letu na matawi mengine yanayo shiriki kwenye maonyesho haya, bendera ya Atabatu Abasiyya imepeperushwa na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, vikiwa na shehena ya vitabu mbalimbali pamoja na kazi za kisanii.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeshashiriki mara nyingi maonyesho haya, pamoja na maonyesho mengine mengi na makongamano ndani na nje ya Iraq, ambayo huendana na mkakati wake wa kusambaza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), mara zote tawi lake limekua likipata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau, huwa na idadi mpya ya vitabu katika kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: