Katika malalo za ndugu zake: Hafla ya kukumbuka kuzaliwa kwa Aqilah Hashimiyyin bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Aqiilah Twalibiyyin bibi Zainabu Kubra (a.s), kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya hafla kubwa katika uwanja wa katikati ya haram mbili na kuhudhuliwa na mazuwaru wengi.

Hafla imefunguliwa kwa Quráni iliyosomwa na Sayyid Badriy Mamitha, ukafuata ujumbe uliotolewa na muongozaji wa hafla (mc) Sayyid Alaa Badriy Awinaat, aliye fafanua ukubwa wa tukio hili tukufu, kwa kueleza maisha ya bibi Zainabu (a.s) na nafasi yake kwa baba yake kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib na mama yake Zaharaa (a.s), akaeleza pia kuhusu uchamungu wake na elimu yake aliyopata katika nyumba ya utume pamoja na mchango wake mkubwa katika harakati ya kaka yake Imamu Hussein (a.s) baada ya tukio la Twafu.

Halafu ukafika wakati wa waimbaji wa tenzi, akaimba bwana Samiri Waailiy na Swahibu Karbala, Hamidi Twawirijawi, na Sayyid Maajid, wakasoma beti za upendo na utukufu wa jabali wa subira bibi Zainabu (a.s) yaliyo jaza furaha katika nyoyo za waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutokana na kumbukumbu ya uzawa huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: